sw.news
61

Waseminari Wa Zamani Wamkengemeka Askofu Wa Hondura Kwa Madai Ya Uzini Wa Kishoga

Edward Pentin amepata ushuhuda zaidi kutoka kwa waseminari wa zamani wa Dayosisi kuu ya Tegucigalpa, Honduras, kuhusu uzini wa kishoga wa Askofu Msaidizi Juan Pineda. Ushahidi huo uliandikiwa upelelezi wa Vatikani uliofanywa na Askofu wa Argentina Alcides Casaretto mnamo mwezi mwaka wa 2017. Tangu wakati huo yamekuwa mikononi mwa Papa Francis.

Dayosisi kuu ya Tegucigalpa huongozwa na Kadinali Oscar Rodríguez Maradiaga, rafiki wa karibu wa Francis na rafiki wa Pineda. Pineda amekuwa kiongozi wa dayosisi hiyo tangu mwezi Januari, kwani Rodríguez hupata matibabu ya kemikali mjini Houston, Texas, kutibu kansa ya tezi-kibofu.

Ushahidi huo una matukio ambayo husemekana yalitendeka wakati Pineda alipokuwa 9akifunza katika seminari. Baadae waseminari hao wawili wa kitambo walilazimika kutoka katika seminari hiyo. Kulingana na shahidi wa kwanza, Pineda alijaribu kuwa na uhusiano wa kingono, "Usiku alikuja karibu nami na kuzishika sehemu zangu za siri na vile vile kifua, nilijaribu kumwachisha, mara kadhaa nilitoka kitandani na kuenda nje."

Shahidi wa pili alitoa ushahidi kuwa alishuhudia moja kwa moja uhusiamo mbaya kati ya Pineda na Mseminari wa tatu. Pineda amesemekana kudumisha msururu wa marafiki wengine wa kiume wa kimapenzi huko Honduras.

Picha: Juan Pineda, © House Committee on Foreign Affairs, CC BY-NC, #newsNlpojldngc