Clicks337
sw.news

Kadinali Marx Apingaye Kanisa Apigana Dhidi Ya Msalaba

Kadinali wa Munich ambaye hulipinga Kanisa Reinhard Marx, akizungumza na jarida linalomilikiwa na matajiri wenye ushawishi mkuu serikalini Süddeutsche alikashifu kwa mara nyingine uamuzi wa Waziri mkuu Markus Söder wa Bavaria, Ujerumani, kubandika misalaba katika nyumba zote za umma.

Kulingana na Marx, uamuzi huu umesababisha "utengano, msukosuko, mzozo" - kana kwamba msalaba umewahi kusababisha jambo lingine.

Alimaanisha kwamba msalaba ulitumika "tu" kama ishara ya mila na kwamba kwa njia hii msalaba "unanyang'anywa kwa jina la taifa".

Katibu mkuu wa CSU, chama cha walio wengi huko Bavaria, alisema kwamba wanaoukosoa uamuzi huo ni "jumuiya ovu ya maadui wa dini na wasiojikubali".

Picha: Reinhard Marx, © Maik Meid, CC BY-SA, #newsXtgjuvovzq