Clicks21
sw.news

Kadinali Marx Hudanganya Usoni Mwa Dunia, "Sikutaka Kuwe Na Baraka Kwa Shoga"

Wakati wa kikao na wanahabari (Februari 19) kabla ya kuanza kwa mkutano wa Maaskofu Wajerumani unaoendelea mjini Ingolstadt, Kadinali Marx wa Munich alishangaza ulimwengu aliposema kuwa "Kamwe sijazungumza kuhusu baraka za hadharani kwa wenzi shoga", ingawaje wakati huo huo alisema kuwa, "Lakini sasa mada hiyo iko hapa."

Huku akicheza na maneno Marx alisema kuwa, alipokuwa akizungumza na Bayerischer Rundfunk mnamo tarehe 3 mwezi Februari, hakuomba "Segnung" (baraka), ila niliomba "Zuspruch", neno la Kijerumani ambalo, haswa miongoni mwa wahuria, hutumika kama kisawe cha "baraka".

Hata hivyo, wakati ambapo kituo cha Bayerischer Rundfunk kilichapisha mahojiano hayo mara ya kwanza chini ya kichwa “Blessing of gay couples is possible” (Baraka kwa wenzi shoga zinawezekana), Marx hakuteta. Mtandao wa maaskofu Wajerumani katholisch.de uliandika mnamo tarehe 3 mwezi Februari, "Marx huzingatia uwezekano wa baraka kwa wenzi shoga". Tena, marx alibaki kimya.

Sasa, ghafla alikana, "Tangazo na kukana" ni mbinu ambayo hutumika na wanasiasa wadanganyifu ili kuwazoesha watu mapendekezo ya kuchukiza na kuyafanya mapendekezo hayo kukubalika katika jamii. Baraka kwa ndoa za kishoga tayari hufanyika katika Kanisa la Ujerumani na Maaskofu kutochukua hatua yoyote.

Picha: Reinhard Marx, © Raimond Spekking, CC BY-SA, #newsNflmrobqyt