sw.news
68

Askofu Ajitoa Uhai

Inaonekana kama Askofu Jean_Marie Balla (58) wa Bafia, nchini Cameroon, alijitoa uhai kwa kujirusha kwenye mto Sanaga. Mnamo siku ya Jumatano adhuhuri, gari lake aina ya Toyota Land Cruiser, lililokuwa limeegeshwa katika daraja la Ebebda, Kilomita 78 kutoka mjii mkuu wa Yaounde, lilionekana na Padre, ambaye alikuwa akisafiria njia hiyo.

Kwenye kiti cha abiria kulikua na stakabadhi za kibinafsi za Balla na barua iliyokuwa imepigwa sahihi "Niko majini". Mwili wake bado haujapatikana. Wandani wa Askofu huyo walikana kuwa Balla alionyesha dalili za kujitoa uhai. Kulingana na mlinda lango, askofu huyo aliondoka kwa gari lake masaa ya saa 5 usiku dhidi ya mtindo wake. Alimwambia mlinda lango huyo kwa kichini-chini kuwa alikua amesafiri kuenda Yaounde.

Picha: Jean-Marie Balla, © Press Picture Diocese of Bafia, #newsYsgwdqqtae