sw.news
75

Ndio, Shughuli Za Siri Juu Ya "Misa Ya Kiekumeni" Zinaendelea

Mvatikani Marco Tosatti amedhibitisha uwepo wa tume ya siri ambayo husimamiwa na Papa Francis ambayo inaunda "Misa ya Kiekumeni," liturujia ambayo inalenga kuwaunganisha Wakatoliki na Waprotestanti …Zaidi
Mvatikani Marco Tosatti amedhibitisha uwepo wa tume ya siri ambayo husimamiwa na Papa Francis ambayo inaunda "Misa ya Kiekumeni," liturujia ambayo inalenga kuwaunganisha Wakatoliki na Waprotestanti altarini.
Akiandika kwenye mtandao wa firstthings.com Tosatti alisema kuwa Katibu [mstaarabu] wa Shirika la Ibada Takatifu, Askofu Mkuu Arthur Roche, na naibu katibu, Monsignor Corrado Maggioni, wamehusika katika baraza hilo. Kinara [Mkatoliki] wa Shirika hilo, Kadinali Robert Sarah, bado hajafahamishwa kuhusu uwepo wa kamati hiyo.
Wengine waliohusika katika mradi huo wa siri ni pamoja na Askofu Mkuu [mstaarabu] Piero Marini na Mliturujia Mlei [mstaarabu], Andrea Grillo, mfuasi mkuu wa Papa Francis.
Picha: © Mazur, catholicnews.org.uk, CC BY-NC-SA, #newsXeqvbyvtmn