sw.news
39

Hatua Itakayofuata Nchini Ujerumani: Ekaristi Kwa Waislamu

Ni "jambo la kawaida" nchini Ujerumani kuwa Waprotestanti walioko kwenye "ndoa kati ya wenzi kutoka kwa kabila au dini tofauti" kupokea Ekaristi, Stephan Orth aliandika kwenye mtandao wa maaskofu wa Ujerumani katholisch.de (February 19). Alitaja kuwa maaskofu hao watakutana juma hili ili kushinikiza Waprotestanti wapatiwe Ekaristi Takatifu.

Kulingana na Orth, ni jambo linaloonyesha "ukosefu wa msimamo thabiti" kwa maaskofu hao kuwa Waprotestanti wanakubalishwa kupokea Ekaristi wakati wa sherehe za harusi na wenzi wao Wakatoliki wala sio baadae.

Hoja hii ni yeneye makosa. Kwanza, Waprotestanti ambao hawana imani katika Ekaristi (vinginevyo wao sio Waprotestanti) na kamwe kutoshiriki katika kitubio, jambo ambalo ni la lazima ili kupokea Ekaristi, kamwe hawajakubalishwa kupokea Ekaristi. Pili, Orth alisema kuwa kwa miongo sasa limekuwa jambo la kawaida katika nchi yake kuwaalika Waprotestanti wote kupokea Ekaristi Takatifu. Hivyo basi wanachokishinikiza maaskofu hao, tayari kipo.

Hili linaonyesha mtinda ambao Ujerumani na kisha Vatina hufuata katika udhoofishaji wa imani ya Kikatoliki: Kwanza wanastahimili dhulma kali kisha wanaendelea "kuzihalalisha".

Ujerumani ni nchi yenye Waislamu weni. NI jambo la wakati tu kisha WAislamu hao wataalikwa kupokea Ekaristi, iwapo bado hawajaalikwa.

Picha: © Jeffrey Bruno, Aleteia, CC BY-SA, #newsOatlxetlpa